top of page

Ramani ya Matokeo: Kwa Ufuatiliaji na Upimaji wa Mipango ya Miradi

Content type:

OM Training Materials

Author(s):

Julius Nyangaga, Fridah Munyi, Elinasi Monga, and the Salvation Army

Theme:

OM Resources: Training Materials

Language:

Swahili

Published:

8 September 2023

Ramani ya kupanga na kupima wa matokeo ni mwongozo wa uandaliaji na utekelezaji wa mradi unaotumia mabadiliko yaliyolengwa kwa wadau kushawishiwa na programu katika mchakato wa kufanya kazi kuelekea lengo linalohitajika. Lengo kuu la programu linategemea jinsi watu mbalimbali wasiowahusika moja kwa moja kwenye utekelezaji wa mradi (wahusika wa kijamii) wanavyoitikia shughuli za utekelezaji wa mradi ili kufanikisha kufikiwa lengo la mradi.

Ni mbinu ya upangaji ambayo ina miongozo ya jinsi maendeleo na mafanikio ya mradi yanavyoweza kufatiliwa na kutathiminiwa. Mwongozo huu unaelekeza jinsi warsha hiyo inaweza kutekelezwa na umetengenezwa kutokana na mwongozo wa awali uliotayarishwa na Sarah Earl, Fred Carden na Terry Smutylo, uliopewa jina la mfumo wa upimaji matokeo; Kuimarisha dhana ya kujifunza na Kutafakari katika Mipango ya Maendeleo, iliyochapishwa na IDRC mwaka wa 2001. Mwongozo huu pia umejumuisha uzoefu wa wadau wengine katika shughuli za upimaji na ufuatiliaji wa matokeo ya miradi ili kuboresha mwongozo huu.

Ramani ya Matokeo: Kwa Ufuatiliaji na Upimaji wa Mipango ya Miradi
bottom of page